Mars ina Maji yanayotembea: NASA imebaini

Mwandishi: Juma Shabani.

Katika utafiti wa hivi karibuni umeoendeshwa na NASA umebaini uwepo wa maji yenye chumvi  yanayotembea katika sayari ya MARS. Utafiti huu umeongeza uwezekano wa uhai kuwepo katika saya hiyo inayotambulika kama sayari Nyekundu.


“Leo, tunafanya mapinduzi ya uelewa wetujuu ya sayari” alisema Mkurugrnzi wa masuala ya sayansi ya sayari wa NASA bwana Jim Green akiwa makao makuu ya Washington. Kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii. “Mars sio kavu, sio jangwa kama tulivyodhani hapo kabla – baada ya mambo kadhaa, vimiminika vya maji vimebainika Mars” aliongeza bwana Jim.

Kwa miaka kadhaa wanasayansi wamekuwa wakitambua kuwa, kwenye sayari ya 
Mars kuna barafu lakini taarifa za kuwepo na maji yanayotembea imechukuliwa kama taarifa ya kupendeza na maendeleo mazuri kuelekea maisha kwenye sayari hiyo.

Mifereji ya giza imeonekana kwenye picha za kiuchunguzi zinazobainisha kutembea kwa maji. Picha hizi zimechukuliwa kipindi cha kipupwe japo vipindi vingene vya mwaka maji haya huganda na kutoweka na mifereji hiyo.

Bi, Mary Beth Wilhelm wa NASA kuhusu uvumbuzi huo amesema “Matokeo yetu inaonesha zaidi jinsi panavyoweza kuwa na maisha katika Mars tofauti na ilivyodhaniwa kabla.”
Jim Green aliongeza “Na sasa tuna nafasi kubwa ya kuwa katika wasaa mzuri wa kuchunguza hilo. (la maisha kwenye Mars)

Kwa uchunguzi huu ni wazi kwamba, katika miaka ijayo au hata karne ijayo. Kuna uwezekano wa binaadam au viumbe hai kuishi katika sayari ya Mars. Kiuchunguzi hii ni hatua kubwa sana nay a kutia moyo.



Chanzo: Fox News

Related

Kimataifa 84738872967126891

Post a Comment

emo-but-icon

Tafuta Habari

Wasomaji

Tufuatilie Facebook

Maoni Yako

Name

Email *

Message *

item
Wordpress