Bugando yaanza upasuaji wa vichwa kujaa Maji kwa watoto.
https://alloycenyanda.blogspot.com/2015/10/bugando-yaanza-upasuaji-wa-vichwa-kujaa.html
DAKTARI bingwa wa kitengo cha mifupa kutoka hospiali ya rufaa ya Bugando bwana Gerald Mayaya amesema zaidi ya watoto elfu 4000 huzaliwa wakiwa na tatizo la vichwa kujaa maji na migongo wazi kati yao 1000 hupata matibabu na 3000 hukosa huduma na kupelekea kufariki dunia.
Akizungumza juzi
wakati wakiwafanyia upasuaji watoto 26 wenye matatizohayo jinsi ya
kuweza kujikinga na maradhi hayo,daktari bingwa wa kitengo cha mifupa Mayaya
alisema matatizo hayo ya kujaa maji vichwa na migongo wazi yamekuwa nitatizo
kubwa yanayopoteza nguvu kazi ya Taifa.
"Ili kukabiliana na
tatizo linalo wakabili watoto,mama anatakiwa kipindi anajiandaa kubeba mimba
anatakiwa kutumia vidonge ya forciasdi na vyakula vyenye kuleta madini hayo
ambayo yanamjenga mtoto pindi anapo kuwa tumboni,"alisema Mayaya.
Aidha Mayaya aliitaka jamii
kuwafichua watoto walio na maradhi hayo ili waweze kupatiwa matibabu mapema
kwakuwa matatizo hayo yanatibika na kumfanya mtoto awe kama wengine endapo
atafikishwa muda muafaka katika kituo cha afya.
Nae mama wa mtoto Faraja
Tido aliyezaliwa na uvimbe mdogo lakini umeleta madhala makubwa na kumpelekea
kufanyiwa upasuaji Atu Ngendelwa alisema wanaume wengi wamekuwa wakowakataa
watoto na kuwatelekeza.
“Mimi nilopo jifungua mtoto wangu alikuwa ana
uvimbe mdogo nilipo mpigia simu mume wangu nikamweleza mtoto anamatatizo
anatakiwa kupelekwa Muhimbili alisema yeye kwao hakuna mtu mwenye matatizo hayo
hiyo simtambui huyo ni wako,lakini nimefika Bugando nikakuta na wanawake
wengine walio na watoto wenye matatizo haya wametelekezwa
NA MANSOUR JUMANNE ,MWANZA