Konisaga : kurejesha fadhila za CCM,Asema bora Lawama kuliko fedheha.



NA MANSOUR JUMANNE,MWANZA

MKUU wa wilaya ya Nyamagana Baraka kunisaga  amemuahidi  Mgombea Mwenza wa nafasi ya kiti cha uraisi  Samia Suluhu,kuwa yeye pamoja na wakuu wa wilaya wenzake wa mkoa wa Mwanza  watahakikisha  wanarudisha  fadhila kwa Chama cha mapinduzi  kutokana nyazifa walizopewa na Chama hicho.


Akizungumza katika viwanja vya shule ya sekondari  Nyabulogoya siku ya Ijumaa  Kunisaga Alimshukuru Samia na Chama Chake kwa Kupewa Ukuu wa wilaya na CCM na amesema hata wao lazime warejeshe Fadhila kwa Chama hicho kwa Kuwaletea Ushindi kwa njia yoyte,ili nao wakistaafu wapate posho zinazo wastahili.

“Nimepewa ukuu wa wilaya na Raisi Kikwete na hivyo lazima hata tutakapostaafu sie Wakuu wa wilaya tupate posho zetu na heshima .

“Sitaki kuondoka na aibu wakati CCM ndo imetupa kazi,kwanza mimi ni mjumbe kamati ya siasa ya wilaya lakini ndio mwenyekiti wa ulinzi na Usalama wa wilaya,hivyo kuanzia sasa mpaka siku ya matokeo kutangazwa matokeo watu wasiwe na hofu”Alisema kunisaga.

Mkuu huyo pia alisema viongozi wa Chadema, bado wanalitaka jimbo la Nyamagana  wamekuwa wakiwahimiza wananchi kuwa baada ya kupiga kura wasiondoke kwenye maeneo ya kuhesabia kura jambo ambalo yeye amesema atahakiksha analishughulikia ipasavyo kama utatokea uvunjifu wa Amani

“Mh mgombea Mwenza mi nakuambia safari hii  bora lawama kuliko fedheha,nimesikia viongozi wa Chadema wanawaambia wananchi wakishamaliza kupiga kura wakae kuzilinda kura sawa,ila wajue tu me na wakuu wenzagu wa wilaya tisa za mkoa wa Mwanza Tumejiandaa vya kutosha “Alisema Kunisaga

Nae Katibu wa Mkoa wa Mwanza CCM, Mtaturu  alipanda jukwaani  na kumpokea microphone  uku nae akisisitiza kwa kusema tayari serikali imeongea hivyo yeye hana la kuongezea hapo.

Related

Tanzania 4821507179430976559

Post a Comment

emo-but-icon

Tafuta Habari

Wasomaji

Tufuatilie Facebook

Maoni Yako

Name

Email *

Message *

item
Wordpress