IRAN NA MAREKANI KWAFUKUTA

Ni baada ya Waziri wa mambo ya Nje Kusalimiana kwa kushikana mikono na Rais Obama.

AFP inataarifu kuwa, Nchini Irani kumeibuka hasira dhidi ya waziri wa mambo ya nje Mohammad Javad Zarif ambaye nje ya mkutano wa umoja wa mataifa uliokuwa unaendelea makao makuu ya umoja wa mataifa UN alisalimiana na rais wa Marekani Bw. Barack Obama.

Hali hii imepingwa vikali na wabunge kadhaa japowasiri amethibitisha kuwa kukutana huko kumetokea kwa bahati mbaya na kwamba haikupangiliwa wao kukutana.

“ Kwa ruhusa ya nani wamekutana na Obama?” Bahram Biranvad alihoji. “mara ya mwisho waliongea na Obama kwenye simu, na mara hii! Kwa ruhusa ya nani? Alihoji bwana Biranvad kuhusu rais Rouhan kuongea na simu na rais wa Marekani.

Zarif pia alikumbana na tuhuma toka kwa msemaji wa mahakama bwana Gholamhossen Mohsen Ejeie kama ilivyotolewa na FARS. Bila kumtaja Zarif, bw. Ejeie alizungumzia suala la kusalimiana na Obama kwa kusema, “Baadhi ya wapelelezi wanalipwa kwa kazi hiyo, ila kuna wengine inabidi tuwape kila kitu kwa kazi hiyo ya kutupeleleza. Anaandaa mazingira ya adui”

Pamoja na makubalina ya July 14 juu ya Nyuklia ya Tehran kufikiwa na nche zenye uchumi mkubwa duniani. Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema Washington itabaki kuwa “adui namba moja wa Iran”

Inataarifiwa kuwa, kusalimiana kwa kushikana mkono huku kwa Zarif na Obama inaweza kuwa mara ya kwanza kunakotambulika kati ya Rais wa Marekani na kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa Iran tangu nchi hizi walipokuwa na mahusiano mabaya ya kidiplomasia tangu mapinduzi ta kiislam ya Iran ya mwaka 1979.

Chanzo AFP


Related

Kimataifa 2416457752745136030

Post a Comment

emo-but-icon

Tafuta Habari

Wasomaji

Tufuatilie Facebook

Maoni Yako

Name

Email *

Message *

item
Wordpress