Kuelekea Oktoba 25: Wasimamizi waaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
https://alloycenyanda.blogspot.com/2015/10/kuelekea-octoba-25-wasimamizi-waaswa.html
Imefahamika kwamba maandalizi muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya
kanda ya ziwa yanaendelea vizuri huku, waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na
maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wakiaswa kuzingatia sheria,
kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato kuelekea Octoba 25 mwaka huu ili
kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara baada ya uchaguzi kumalizika.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku mbili iliyo andaliwa na Tume ya taifa ya uchaguzi na kuhusisha Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi, na maafisa uchaguzi kutoka katika mikoa ya Mwanza na Mara Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Manju Msambya, amesema watumishi hao wanayo dhima ya kuhakikisha zoezi la uchaguzi linakwenda vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Msambya amesema nilazima dhamana waliopewa watumishi hao watambue
ni muhimu kwakua inakwenda kutoa mustakabali wa taifa letu na wapi tunako
taka kuelekea kwa kuchagua viongozi kwa nafasi za udiwani, ubunge na urais.
“Ndugu wanasemina tambueni kwamba, madhumuni ya semina hii nikuwajenge uwezo
katika mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea, upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha
pamoja na kutangaza matokeo ya uchaguzi” hivyo suala la umakini ni muhimu sana.
Msambya amesema, kwakutumia uzoefu walionao watumishi hao katika
mazoezi mbali mbali ya kitaifa wataweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa
hasa ikizingatiwa kwamba wengi wao walishiriki katika zoezi kama hilo kwa mwaka
2010.
Awali akimkaribisha kufungua semina hiyo Mratibu wa uchaguzi wa
kanda ya ziwa Deogratius Nsanzugwanko alisema tayari maandalizi kadhaa
kuhusiana na uchaguzi yamekwisha kamilika ikiwapo madaftari ya mikoa ya kanda
ya ziwa pamoja na vifaa vyote muhimu kuwa tayari vimekwisha anza kusafirishwa
kwenda kwenye mikoa husika.
Kanda ya ziwa inayoundwa na mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera,
Simiyu na Mara, ambapo kwa mkoa wa Mwanza pekee inakadiriwa kuwa na wapiga kura
1,442,391 sawa na asilimia 103% ya lengo lililokuwa limewekwa hapo awali na
bodi ya takwimu ya mkoa wa Mwanza ya kuandikisha wapiga kura 1,403,763.