TANZANIA YAPANDA VIWANGO FIFA, LAKINI WAPI BADO KIBONDE AFRIKA MASHARIKI NA KATI.
https://alloycenyanda.blogspot.com/2015/10/tanzania-yapanda-viwango-fifa-lakini.html
Tanzania imepanda nafasi nne katika
viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lakini bado hali
yake ni mbaya kwa jumla katika takwimu hizo zilizotolewa jana Alhamisi.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya 136 ikiwa ndiyo nchi ya chini kwa ubora kati ya zile zilizopo Afrika Mashariki katika chati hiyo.
![]() |
| Kikosi cha Taifa Stars (Picha: Maktaba) |
Argentina
imeendelea kubaki namba moja ikifuatiwa na Ujerumani ambayo imepanda kwa nafasi
moja ikiishusha Ubelgiji iliyoshika nafasi ya tatu. Ureno imesogea mpaka nafasi
ya nne wakati kwa nchi za Afrika inayoongoza ni Algeria ikiwa nafasi ya 19.
Viwango vya Fifa
1. Argentina
2. Ujerumani
3. Ubelgiji
4. Ureno
5. Colombia
6. Hispania
7. Brazil
8. Wales
9. Chile
10. England
75. Uganda
93. Rwanda
113. Burundi
131. Kenya
136. Tanzania
