SERENA AFUNGA MWAKA,Ajiondoa mashindano ya China Open na Fainali za WTAza Singapore


Mamlaka ya mashindano ya China yalitoa ujumbe kwa njia ya tweeter wakithibitisha, lakini Umoja wa Tennis ya wanawake haijathibitisha taarifa ya Serena kujiondoa katika mashindano hayo.
Inaarifiwa kuwa mchezi namba tatu kwa ubora wa mchezo huo kwa wanawake Maria Sharapova nae ametangaza kujitoa kutokana na majeraha ya sehemu ya mbele ya mkono wake wa kushoto.
Serena mwenye miaka 34 hajacheza mchezo wowote tangu aliposhindwa kwenye nusu fainali ya US Open kwa muitaliano Roberta Vince moja ya matokeo ya kushitusha zaidi katika mchezo huo.
Serena alisema “si siri, nimecheza sehemu kubwa ya mwaka huu nikiwa na maumivu… yaweza kuwa kiwiko, fundo la mguu na sehemu kadhaa maumivu makali”
Mwalimu wa serena, Patrick Mouratoglou alieleza mapema wiki hii kuwa, Serena amefedheheshwa sana na matokeo ya US open yaliyopelekea kutoshinda shindano la tano mfululizo na akatahadharisha kuwa angejitoa kwenye mashindano mengine.
Pamoja na kujitoa mashindano mawili ya kuhitimisha mwaka huu, Serena ataumaliza mwaka huu akiwa mchezaji namba moja kwa wanawake katika mchezo huo.
Kujitoa kwa Serena Williams kumewahuzunisha watu wengi kwenye mchezo huo akiwemo aliyemshinda kwenye US Open Vinci mwenye miaka 32 ambo[po alisema “Nampa pole Serena, lakini Serena ni Serena na kwamba bado ni mchezaji bora hata asipocheza”

Souce AFP


Related

Michezo na Burudani 3782453755128209441

Post a Comment

emo-but-icon

Tafuta Habari

Wasomaji

Tufuatilie Facebook

Maoni Yako

Name

Email *

Message *

item
Wordpress