Ojadact :Sheria za Utangazaji Zimekanyagwa

Chama  cha  waandishi wa  habari wa kupiga  vita  matumizi  ya  dawa za kulevya  na uhalifu tanzania (ojadact) kinachukua  nafasi  hii  kuongea nanyi waandishi wa habari  juu  ya sheria ya  maudhui  ya  utangazaji ( the  broadcasting  services  content).



Ndugu waandishi wa habari  tunaelewa kuwa, mamlaka  ya  utangazaji  tanzania (tcra) ni  chombo  kilichoundwa  kisheria  na kina wajibu wa kusimamia  sekta  ya utangazaji  nchini  kama jinsi sheria no 12  ya mwaka 2003  iliyounda   chombo  hicho.

Kwa masikitiko makubwa  tunawaambia  ndugu waandishi wa habari  kuwa,  sheria ilitangazwa  kwenye  gazeti la serikali  Juni 26, 2015  na kuanza  kutumika, heria  hii  imekuwa ni  kitanzi  kikubwa  kwa tasnia  ya habari  nchini  kwani  inanyima  uhuru  wa  vyombo vya  habari (M&F) na haki  ya  kupata   habari(RTI)   wakati wa kuelekea  kwenye  uchaguzi mkuu wa  Oktoba 25 mwaka  huu,  kama zilivyo  sheria  za makosa ya  kimtandao  na takwimu  za mwaka 2015 pamoja  na miswada  ya  sheria  ya  haki ya  kupata  taarifa na  ule wa huduma za  vyombo vya  habari ambayo  ilizuiliwa  kujadiliwa bungeni  mwezi Juni, 2015.

OJADACT  tumeitazama sheria  ya  maudhui ya  utangazaji(Broadcasting  services) na kuona mapungufu    yafuatayo:-

·         Sheria  hiyo  haijahusisha  wadau  wa habari,  kama  miongozo ya utungaji wa sheria ndogo au kubwa  unavyotaka,  jambo linalotia  shaka  na kupelekea  kuwa kati ya   sheria   kandamizi  zinazotungwa kwa lengo lakuminya  uhuru  wa  vyombo  vya  habari  na haki  ya  kupata  taarifa(Infringe  media  freedom and  right  to information).

·         Sheria hiyo  ina inageuza   wajibu wa misingi ya kitaaluma  kuwa  matakwa  ya  kisheria  na hivyo  kufuta  maana  ya weledi   katika tasnia  ya  habari,  mfano  kusisistiza  kazi na wajibu wa mwandishi kutekelezwa  kisheria. Rejea  sehemu  ya  pili ya sheria  kifungu cha 4(a,b,c,d,f, na na g).

·         Sheria  hii  inaingilia   weledi  wa tasnia  ya  habari kwa kutotambua  baadhi  ya  vigezo vilivyowekwa  na wanataaluma  kama chanzo  cha  habari(News  values), kwani  haitambui chanzo  cha mtu  katika kutengeneza  habari(Prominence). Rejea  kifungu cha 4(i) ambapo kifungu  hicho  kinakataza vyombo vya  habari  kuripoti  tukio/matukio ambayo yanamhusisha  mtu moja kwa moja  bila  kujali kuwa  yawezekana  tukio  la mtu likatengeneza  habari  na kuwa  na maslahi kwa umma.

·         Sheria  hiyo  ina mkanganyiko  kati  ya  sehemu  za utangulizi  na vifungu  vinavyobeba  maudhui husika.(Rejea sehemu ya III kifungu cha 15 ) kwenye  utangulizi maneno yanasomeka  No broadcast on poling day na  kwenye  kifungu  cha maudhi  cha 15 (2)kinafafanua  kwamba, twelve   hours immediately  proceeding  polling  day, they  do not broadcast any politically – related  matter which may  reasonably  upset the  balance to  be  observed throughout  the  election  broadcast period pursuant  to this  code.

·         Sheria imeweka mitego mipana  na maana  ya  mambo  ambayo hayatakiwi, Mfano  kifungu  cha 15 (2) maneno yafuatayo.. No  broadcast any  politically – related  matter  which  may  reasonable  upset the  balance  to be  observed …… Hapo ni wazi  kuna mkizano wa maana  pana inayoweza kutafsiriwa na mamlaka moja tu  yani watunga  sheria  na sio  watumiaji wa sheria.

·         Sheria  pia  imenyakua  miongozo   ya kitaaluma  kwa mwandishi na kuifanya sheria  badala   kuiacha  katika  maadili ya  kitaaluma (Media  ethics)  ambayo ingeweza kusimamiwa  na  vyombo  husika  kama MCT, UTPC, OJADACT, MISA, TAMWAN na vingine. Rejea  msisitizo wa  sehemu  ya  II kifungu  cha 4(a) – (i)

RAI:
·         Kuwe  na maridhiano  ya  pamoja  baina  ya  TCRA  na wadau wa habari   ili  kutazama   utekelezaji wa  sheria  hii  ili  kutominya  uhuru  wa  vyombo  vya  habari na  haki  ya kupata  taaifa  kwa wananchi.
·         Serikali  iache  kuwa  na ajenda  ya  siri  katika  kuvibana  vyombo  vya  habari  wakati huu  wa kuelekea kwenye  uchaguzi  mkuu badala  yake  ishirikiane  na  vyombo  hivyo  kutengeneza  ajenda  ya  kuwavusha  watanzania salama  kwenye  uchaguzi  huu.
·         Wamiliki wa vyombo vya  habari na waandishi wa habari  wawe makini  na sheria  hii


MSIMAMO WA CHAMA
Sheria  hii  siyo  rafiki  kwa  vyombo  vya  habari  na inalenga  kuvibana   vyombo  hivyo  kutofanya  kazi  iapasavyo  kuelekea  uchaguzi  mkuu wa  mwezi  Oktoba, 25  mwaka huu,  kama  zilivyo  sheria  nyingine kama ifuatavyo sheria  ya    makosa  ya  mtandaoni na takwimu  zinazoanza  kutumika  mwezi  Septemba 1, mwaka  huu  ina  ile  miswada  miwili  ya haki ya  kupata  taarifa  na  huduma  kwa  vyombo  vya  habari.
Description: cartoon_b1Press Freedom.JPG






Description: Closing cartoon.jpg






                                       
Edwin   Soko
Chairperson
           


Related

Tanzania 3818069805730764239

Post a Comment

emo-but-icon

Tafuta Habari

Wasomaji

Tufuatilie Facebook

Maoni Yako

Name

Email *

Message *

item
Wordpress