Katika match ya jana Cristian
Ronaldo aliandikisha magoli mawili katika mchezo huo na kufikisha idadi sawa ya
magoli ya kufunga na Raul. Katika mshikemshike wa jana, Ronaldo aliifungia Real
Madrid magoli hayo na kuandikisha jumla ya magoli 323 sawa na Raul aliyeichezea
Madrid zaidi ya match 400 kufikisha idadi hiyo huku Ronaldo akiwa amecheza
mechi chache kufikisha magoli hayo.
Pia ronaldo amefikisha zaidi
ya magoli 500 katika michuano yote aliyocheza. Ronaldo aliyesajiliwa kutokea
Manchster United aliyoichezea kati ya mwaka 2003 na 2009 kabla hajajiunga na
miamba hiyo ya jiji la Madrid kwa uhamisho wa $90 million au Pound 59million.
Alipoulizwa kuhusu kuihama
Real Madrid kuelekea timu yoyote alijibu ifuatavyo”Nina furaha hapa, nataka
kushinda kila kitu hapa. Ninajisikia vizuri hapa, ila kama nilivyowahi kusema
zaidi ya mara million, hakuna mtu anayejua yatayotokea siku za mbele” aliyaongea
hayo alipokuwa akiongea na Cadena SER
“ Tutaona yatayotokea kesho,
ila kwa sasa, nina furaha ndani Real Madrid” Aliongeza
“hakuna anayejua yatayotokea
mwaka ujao. Nina furaha hapa, ila huwezi jua yatayotokea mbeleni”
“Natakiwa kufikia malengo
Fulani hapa, Ninajisikia vizuri, ninataka kushinda vitu na Real Madrid kwakuwa
ninadhani kilabu hii inanafasi ya kushinda mashindano, ila sijui yatayotokea”
Maelezo haya ya Ronaldo
yanaiweka Real Madrid katika wakati mgumu maana anaweza kuondoka na kuelekea
vilabu kadhaa ambavyo vimeonesha kumuhitaji. Ambapo amekuwa akihusishwa na
kurudi Manchester United, huku PSG na Machester City wakimtolea macho pia.
Alipoulizwa kuhusu dhihaka za
mchezaji wa team hasimu ya Barcelona kuhusu kukutwa kwake sehemu ya starehe
baada ya kushindwa alijibu “ si muda sahihi kuongelea mambo haya. Siongelei
hili kwakuwa si kitu sahihi, kwahiyo kila mtu anaweza kufikiria atakavyo”
“ilikuwa maamuzi yangu.
Sikutaka kuliongelea na hakuna mtu naelazimika kujieleza kwake. Naongea
napojisikia kuongea, hata team yangu haijawahi kunilazimisha kuongea.”
Alipoulizwa kwanini haongei
mara nyingi na vyombo vya habari aliji, “Kwanini siongei mara kwa mara? Ni kwa
sababu maswali mnayouliza sio mazuri. Sasa hili la kwenda kwenye starehe na
Roldan linahusiana nini na mchezo?” “Mnataka mniweke kwenye tatizo kama Pique
alivyofanya, Kwanini inihusu?”
Real Madrid imejiweka katika
nafasi nzuri ya kuvuka makundi katika kombe la EUFA baada ya kushinda michezo
miwili za makundi.
Mwandishi Juma…