MNYAMA USIPOWALA UTAENDELEA KULIWAA ,MPENI MO CLUB
https://alloycenyanda.blogspot.com/2016/08/mnyama-usipowala-utaendelea-kuliwaa.html
kwa Mashabiki wa Club ya Simba bila shaka ni mateso makubwa kuwa shabiki wa timu ya Simba kwa kipindi hiki. Huu ni msimu wa nne sasa club ya Simba haijashiriki michuano ya kimataifa. Lazima ukumbuke Simba ni timu yenye sifa hiyo, kushiriki na kufanya vizuri nje ya Tanzania.
Rekodi zinaibeba kwenye mambo mengi sana simba Timu ambayo imefanya vizuri zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki katika michuano yenye ushindani
Ndiyo timu pekee ya Tanzania kufikia fainali ya michuano mikubwa zaidi kwa upande wa klabu. Hii ni kwa Afrika Mashariki yote, wao ndiyo pekee wamecheza fainali ya Kombe la Caf mwaka 2003.
Hata iwe vipi, lazima tukubali, Simba kufeli kwa misimu minne si jambo dogo hata kidogo. Simba si kama Ndanda au Simba si kama Toto ambayo wakati ilikuwa inachangiwa hadi maji ya kunywa na wachezaji wake wanashinda milima wakisubiri mechi ya ligi kuu kwenye uwanja wa ccm kirumba hii hatari,hata kula tabu (Hill la Toto Nimechomekea) lakini ukweli wamechokaaa kweli.
Sote tufahamu Wekundu wa Msimbazi ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyofanikiwa kucheza fainali za Kombe la Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika yaani CAF. Ilikuwa mwaka 1993 wakati huo likijulikana kama Kombe la Caf.
Simba ilicheza fainali hiyo na Stella Abidjan ya Ivory Coast na kutoka sare katika mchezo wa awali kabla ya kukubali kipigo cha mabao 2- 0 katika marudiano jijini Dar es Salaam.
Licha ya Simba kupoteza mchezo huo ambapo wachezaji wake waliahidiwa zawadi za magari kama wangeshinda, inasalia kuwa timu pekee kutoka Tanzania Bara iliyofanikiwa kucheza hatua hiyo ya fainali hizo.
Nusu fainali klabu Bingwa Afrika
Historia ya klabu ya Simba inavutia! Ndivyo unavyoweza kusema kwa lugha rahisi baada ya timu hiyo kufanikiwa kucheza nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1974.
Hata hivyo iliondolewa katika hatua hiyo ya nusu fainali na klabu ya Mehala El Kubra ya Misri na kuzima ndoto za kucheza fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi katika bara la Afrika.
Rekodi hiyo ya Simba bado haijavunjwa mpaka leo hii ni timu yoyote ya Tanzania, japo mwenendo wake kwa sasa wasipofanya maamuzi sahihi ziyavunjwa tu na hata nyegezi vetelani
Mbali na rekodi tajwa hapo juu ambazo huenda zikazidi kuchagiza machungu kwa mashabiki wa timu hiyo. Simba SC bado inajivunia rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kufanikiwa kuiondosha timu ya Misri katika michuano ya Afrika.
Wanaume hawa walifanya hivyo mwaka 2003 baada ya kuifunga Zamalek ya Misri ambayo ilikuwa inatetea ubingwa huo.
Ni kweli rekodi na takwimu hizi tamu zinaifanya Simba ibaki kuwa na historia nzuri na ya kuvutia kimataifa lakini kwa sasa haina jipya kutokana na mwenendo wake usiotia matumaini.
Sasa Kuna kawimbo ka msanii mpya anaitwa sadimu kibao kimeimbwa kwa madaha kweli kinasema SASA IMEKI HISTORIA ,Ili isiwe hivyo Mpeni Timu Huyo mwekezaji MO aweke bajeti ya Billion 5 kwa mwaka ili muachane na omba omba ,Mtafukuzwa Dar makonda hataki omba omba na wasio na kazi .
Naomba nieleweke mimi so shabiki wa Simba ni mpenzi wa Rekodi ya Simba ,ila mfahamu mimi ni mchezaji wa Club ya Sahara sport tena mchezaji wa kutumainiwa wachezaji wenzangu hupenda kuniita pogba lakin Mimi hupenda kuitwa Crespo
Kwa nijuavyo mimi, hakuna linaloshindikana chini ya Jua. “Ni kweli imebaki historia! Ngoja tuusubiri msimu mpya wa Ligi huenda ikaja kivingine.
Alloyce nyanda


