Wanasiasa walipuuza kitisho cha viruii vya corona
https://alloycenyanda.blogspot.com/2020/03/wanasiasa-walipuuza-kitisho-cha-viruii.html
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amekiri hii leo kwamba viongozi wa kisiasa walipuuza ukubwa wa hatari ya virusi vya corona katika wakati ambapo umoja huo unachukua hatua kufunga mipaka yake.
Von der Leyen ameliambia gazeti la Bild la Ujerumani kwamba anadhani viongozi wote ambao si wataalamu awali hawakuuchukulia kwa uzito mripuko wa virusi vya corona, lakini sasa inaonekana wazi kwamba virusi hivyo vitawashughulisha kwa muda mrefu ujao. Hata hivyo von der Leyen ameipinga lugha ya rais Emmanuel Macron ambaye mapema wiki hii aliufananisha mripuko huo na vita na kuwaagiza watu karibu wote kubaki nyumbani angalau wiki mbili akisema asingependelea kutumia neno hilo ingawa anaelewa hamasa ya rais Macron kwa sababu virusi hivyo vimekuwa adui anaetia wasiwasi. Waziri wa uchumi wa Ujerumani Peter Altimaier amesema Marekani chini ya Rais Donald Trump imekichukulia kitisho hicho hata kwa urahisi zaidi.