Uongozi DP waitaka Serikali kufuatilia kwa makini chanzo kifo cha mtikila
https://alloycenyanda.blogspot.com/2015/10/uongozi-dp-waitaka-serikali-kufuatilia.html
Chama cha Democratic DP kimeiomba Serikali na vyombo vya
dola kufuatilia kwa kina chanzo cha kifo cha mwenyekiti wa chama hicho
Mchungaji Christopher Mtikila kufuatia kuibuka utata wa kifo hicho
kilichotokea kwa ajali ya gari Octoba NNE mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu
Naibu Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya amesema wameshangazawa na
kushtushwa na ajali hiyo na wanafikiri ni ajali ya kupangwa
Naibu Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya amesema Mchungaji
Mtikila alidai kufuatiliwa na gari za aina tofauti tangu alipokuwa
akielekea mjini Mwanza kwenye kipindi baada ya kumaliza mikutano mjini
Bunda Septemba 25 na 26 mwaka huu .
Hata hivyo ameeleza kusikitishwa kwao na baadhi ya picha
zilizopigwa katika eneo la ajali huku wakiwa na maswali mengi juu ya
aliyepiga picha hizo.
Mchungaji Patrick Mgaya ambaye alikuwa na marehemu kwenye
gari wakati ajali inatokea amesema walikuwa wakifuatiliwa na gari aina
ya Toyota Land cruza kutoka Mafinga mpaka ajali ilipotokea.
Mwili wa mchungaji Mtikila utaagwa kesho saa 3 asubuhi
jijini Dar es salaam katika viwanja vya Karimjee na baadaye
utasafirishwa kupelekwa Ludewa, Iringa kwa mazishi.
Miongoni mwa madai aliyokuwa akidai Mchungaji Mtikila ni pamoja na Tanganyika yake.
