Maafa ya Mahujaji Makka yaongezeka
https://alloycenyanda.blogspot.com/2015/10/maafa-ya-mahujaji-makka-yaongezeka.html
Nchi ya
Irani inasadikiwa ndio iliyopata maafa makubwa kwenye maafa yaliyotokea Hijja
ya mwaka 2015 kutokana na kukanyagana kwa mahujaji huko Minnah. Habari za idadi
ya mahujaji ilipanda ghafla jumatano hii ambapo Irani ilitangaza mahujaji wa
kiirani wapatao 465 walipoteza maisha katika tukio hilo hali inayopelekea mahusiano
yasiyoridhisha kati ya mahasimu hao wawili Iran na Saudi Arabia.
Wakati
tawala ya Saudia ilitangaza mahujaji 769 kupoteza uhai, Mashirika ya
kitangazaji yakihusiana nay a maafa ya kila nchi yalionesha wastani wa mahujaji
999 walitoweka karibu na mji mtakatifu wa Makka.
Makadiro
yanaonesha kuwa maafa ni makubwa zaidi kwani uchunguzi wan chi 15 tu zilizopata
maafa umetumika huku nchi zaidi ya 180 zilipeleka mahujaji wanaofikia million
mbili katika hijja ya mwaka huu.
Nchi za
Pakistan, India, Indonesia na Iran zote zimedai kuwa maafa yanaweza kuwa juu ya
ilivyotangazwa na ufalme wa Saudia.
Mkurugenzi
wa mawasiliano wa wizara ya afya bwana Faisal Alzahran, aliiambia AP Jumatano
hii kuwa, ofisi yake inaidadi ya waliofariki 769 na majeruhi 934 waliojeruhiwa
Minnah. Alieleza kuwa, mamlaka za kiusalama zitaendelea kutangaza kwa kadri
idadi itavyoongezeka wakati zikendelea kuchunguza sababu za maafa hayo.
Katika nchi
zote, Iran inaonekana ndio iliyopoteza mahujaji wengi zaidi. Kulingana na
taarifa iliyotolewa na AP, idadi ya watu 600 kutoka duniani kote wamepotea
baada ya tukio la Septemba 24.
Baada ya
Iran, nchini zingine zilizopata maafa ya mahujaji ni pamoja na; Misri watu 124,
Nigeria watu 64, Mali watu 60, Pakistan watu 52, India watu 51, Cameroon watu
42, Bangladesh watu 41, Ethiopia watu 13, Chad watu 11, Kenya watu 6, na
Tanzania ikiandikisha watu 5 waliofariki.
Taarifa za
leo hii kutoka Jakarta Indonesia zinaeleza kuwa Mahujaji 91 kutoka nchini humo
na wengine 38 hawajulikani walipo. Kulingana na idadi kubwa ya Mahujaji
kupotea, mpaka sasa inasadikiwa walioaga dunia kufikia 1036.
Haya ni
maafa makubwa sana kwa miaka ya karibuni kutokea huko Makka wakati wa hija na
imeinua hali ya kutoaminiana kati ya Iran na hasimu wake Serikali ya Kifalme ya
Saud Arabia.
Inna Lillah,
wainna ilayh rajiun. Kwa majeruhi, Mwenyezi Mungu awajaalie wapone haraka na
kwa waliopotea, Mwenyezi Mungu ajaalie wapatikane wakiwa hai. (Amiin)
Mwandishi: Juma Shabani
