Ndege ya Marekani yatua ghafla baada ya rubani kufariki.
https://alloycenyanda.blogspot.com/2015/10/ndege-ya-shirika-la-ndege-la-marekani.html
Ndege ya
Shirika la ndege la Marekani aina ya Airbus yenye namba A320 ambayo ilikuwa na
abiria 147 iliyokuwa ikitokea Phoenix kuelekea jiji la Boston ililazimika kutua
kwa ghafla Syracuse baada ya rubani mmoja kati ya wawili kupata ugonjwa na
hatimaye kuaga dunia safarini. Ndege hiyo ilitua salama saa 1 asubuhi.
Na Juma Shabani
Rubani huyo
ambaye, umri, jinsi na jina lake havijawekwa wazi mpaka sasa alianza kuumwa na
kupewa huduma ya kwanza na nesi ndani ya ndege akisaidiana na wahudumu wengine.
Jitihada za kuokoa maisha yake zilishindwa na kupelekea kifo cha rubani huyo
hali iliyopelekea rubani aliyebaki kuamua kuishusha ndege kwa dharura.
Shirika la
ndege lilisema, “tukio hilo ni la kusikitisha” na sasa wanaangalia juu ya
kuihudumia familia ya rubani na wafanyakazi” iliripoti ABC.
Sheria za
Marekani, zinalazimisha mashirika yote ya ndege kuwa na marubani wawili kila
ndege inaporuka. Msemaji wa shirika alisema “Kwa kiasi kikubwa tumejiandaa
kushughulikia hali kama hizi zinapotokea.” Ndio maana kunakuwa na rubani zaidi
ya mmoja kwenye ndege” alihimisha msemaji.
Habari hii
imeandaliwa kwa msaa wa ABC na BBC.
Na Juma Shabani
Chanzo BBC
