Rais Kikwete kulihutubia Bunge la Kenya.

Rais anayemaliza muda wake wa Tanzania atakuwa mgeni wa heshima wa kwanza kulihutubia Bunge la Kenya atapoitembelea Kenya wiki ijayo.
Spika wa Bunge Justin Muturi amelitaarifu Bunge juu ya ratiba ya kukutana kwa seneti siku ya jumanne ya wiki ijayo. Inatarajiwa Kikwete kuwa atatumia fursa hiyo kuiaga Kenya kupitia Bunge hilo.
Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu wake Oktoba 25 mwaka huu. Ilitarajiwa Rais wa Marekani Barack Obama angelikuwa rais wa Kwanza wa nje kulihutubia Bunge hilo la 11 alipoitembelea Kenya, lakini ilishindikana dakika za mwisho kwa kile ilichodaiwa kuwa hofu ya kiusalama.
 
Rais Kikwete
Hivi karibuni Kikwete aliielezea kazi yake kama “kazi inayowazisha na ngumu” akiongeza kuwa, alikuwa akiomba sana kipindi chake kiishe. “Vipindi viwili vinatosha” Alisema akiwa Woodrow Wilson International Centre for Scholar, Washington DC mapema mwaka huu.

Katika Kipindi hicho pia, Rais Kikwete alieleza kuwa “Baada ya miaka 10, unahitaji kuendelea na maisha mengine. Imekuwa miaka 10 tangu niwe katika wadhfa huu mkubwa zaidi, Nilikuwa nina miaka 55 tu, ila nachoweza kukueleza, kazi hii inaumiza sana akili na inachosha”

Rais wa Tanzania yuko nchi kenya katika ziara mbalimbali za kuaga, kabla ya kufikia ukomo wa uongozi wake mapema mwaka huu mara baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25

Mwandishi: Juma Shabani

Related

Tanzania 625077341453090719

Post a Comment

emo-but-icon

Tafuta Habari

Wasomaji

Tufuatilie Facebook

Maoni Yako

Name

Email *

Message *

item
Wordpress