TANAPA watoa tamko kuhusu mamia ya Nyumbu kufa

TANAPA watoa tamko kuhusu mamia ya Nyumbu kufa Mto Mara,Serengeti wasema Matukio ya vifo vya nyumbu ni ya kawaida katika maisha ya wanyama jamii ya nyumbu
Shirika la Hifadhi la Taifa, TANAPA, limetoa ufafanuzi kuhusu habari iliyochapishwa na tovuti ya Africa Geographic Septemba 28, 2015 iliyosema mamia ya nyumbu wamekutwa wakiwa wamekufa Tanzania








Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na TANAPA ilisema taarifa ya wavuti hiyo iliambatanisha na picha za Mto Mara zikionyesha mizoga ya nyumbu hao ambapo taarifa ya wavuti hiyo ilinukuliwa ikisema Mamlaka husika (TANAPA) bado haijathibitisha idadi kamili ya vifo.
Ufafanuzi:
Kwa mujibu wa taarifa ya TANAPA, kuhama kwa Nyumbu Serengeti ni jambo ambalo hutokea kila mwaka. Mamilioni ya Nyumbu na Pundamlia huhama kutoka Mbuga ya Serengeti nchini Tanzania kuelekea Maasai Mara iliyopo Kenya kutafuta maji na malisho.
Katika kuhama huko, maafa huweza kutokea na kuzama ndani ya Mto Mara ni kati ya ajali ambazo huweza kutokea. Inakadiriwa kuwa zaidi ya nyumbu 250,000 hufa katika kipindi hiki.
Pamoja na hayo, vizazi vipya zaidi ya 350,000 hutokea kila mwaka hivyo kufidia idadi ya waliopotea wakati wa kuhama kati ya mbuga hizo mbili.
Kwa kuzingatia hayo, Shirika linautaarifu umma kuwa vifo vilivyotokea ni sehemu ya maafa ambayo huwa yanatokea katika kipindi kama hicho kila mwaka, hakuna ambacho wangeweza kufanya kama shirika kuzuia vifo hivyo.
 Chanzo:Cloudsfm.com
Mwandishi wetu kitaifa

STANSLAUS CHACHA




Related

Tanzania 4500983107565231375

Post a Comment

emo-but-icon

Tafuta Habari

Wasomaji

Tufuatilie Facebook

Maoni Yako

Name

Email *

Message *

item
Wordpress