Watekelezaji wa sheria ya makosa ya mtandao wapewa mafunzo.
https://alloycenyanda.blogspot.com/2015/10/watekelezaji-wa-sheria-ya-makosa-ya.html
NA MANSOUR JUMANNE,-MWANZA.
Wizara ya Mawasiliano,Sayansi, na Teknolojia imeanza kutoa mafunzo
rasmi kwa makundi mbalimbali ya watekelezaji wa sheria ya makosa ya mtandao
na sheria ya Miamala ya kielektroniniki ili kuwajengea uwezo
wa utekelezaji wa sheria hizi katika kuzuia uhalifu wa
mtandao, uchochezi, udhalilishaji, utumiaji ujasusi data, pamoja na utumaji
wa picha chafu.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Mwanza kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya mawasiliano, Prisca
Ulomi ambaye ni msemaji wa wizara hiyo, alisema makundi
yaliyohudhulia mafunzo hayo ni pamoja Mahakimu,Waendesha Mashtaka, Maofisa kutoka
jeshi la polisi na ofisi ya mwansheria mkuu wa serikali kutoka mikoa ya
Mwanza, Geita, Simiyu, pamoja na Mkoa wa Mara.
“Sasas hivi watu wanafanya wizi wa mitandao ,watu wanatumia
mawasiliano kuiba kwenye mabenki, mtu anaweza kuwa nchi nyingine na akaiba
fedha kwenye nchi nyingine kwa kutumia mitandao, lakini kuna utumiaji wa picha
za ngono, udhalilishaji, uchochezi hivyo lengo letu kama wizara
ni kuhakikisha makosa haya yanakwisha kabisa kama si kupungua ,” Alisema
Prisca.
Kwa upande wake mwanasheria wa wizara hiyo, Bi Yunus Masigati,
alieleza juu ya Sheria ya mtandao ya Mwaka 2015 pamoja na Sheria ya miamala ya
ya kielektroniki ya mwaka 2015 alisema sheria hizi hazikuja kwa sababu
ya uchaguzi bali sheria hizi zilianza kufanyiwa kazi mwaka 2003 Chini ya sera
ya TEHAMA,
“Sheria hizi hazikuja kwa ajili ya Uchaguzi kama wengi wanavyosema
,sheria hizi kwetu zina faida kiuchumi,lakini sheria hizi zinatulinda juu ya
wale wahujumu miundo mbinu ya “TEHAMA” ambayo adhabu yake wakikamatwa
ni Shilingi milioni 100, kifungo cha miaka mitano au vyote kwa
pamoja,lakini sheria hizi zinatuwezesha kulinda utu wa binadamu, pamoja
na kupunguza uharifunchini Tanzania”Alisema Yunus.
Nae Mwanasheria kutoka jeshi la Polisi nchini Tanzania
Bwana Alfred Ahonga, alisema Jeshi la polisi tayari linayo mitambo ya kutosha
na tayari walikwisha toa mafunzo kwa vijana wa jeshi la polisi ili wawe
wapelesi wazuri kwa ajili ya kuwabaini Waharifu wa mitandao.
Pamoja na kuahidi kutenda haki pia washiriki wa mafunzo hayo
walisema wameyapokea vizuri mafunzo hayo na sheria hizi zitawasaidia
zaidi katika kuamua makosa ambayo yatakuwa yanajitokeza katika mitandao.

Napendekeza bwana Nyanda ukisha itupia kwenye Blog uwe una share kwenye Mitandao mingine kwa ajili yakuiuuza Blog
ReplyDelete